Loading...
Taarifa ya Habari

‘Kuwasha Taa la Elimu na Ushindi Dhidi ya Saratani ya Matiti - Saifee Marathon’

Mwezi wa 10 huleta mwangaza kwa jamii duniani kote kuhusu ugonjwa wa saratani ya matiti. Kwa Tanzania, saratani hii ni ya pili kwa kujitokeza miongoni mwa wanawake wetu. Katika muktadha huu, wengi wetu bado hatuna elimu sahihi kuhusu dalili na ugonjwa huu, na hofu kubwa inawakumba wanaopima afya zao kwa sababu ya imani potofu kwamba saratani ya matiti ni hukumu ya kifo.

Hata hivyo, Hospitali ya Saifee Tanzania inaleta mwanga kwa jamii yetu. Tunatamka kwa sauti kubwa: "Ukiwa na ujasiri wa kufanya uchunguzi na ukagundulika na saratani mapema, unaweza kupona." Hivyo, kwa lengo la kusaidia jamii na kusambaza elimu, tumekuwa na hamasa ya kipekee - Saifee Marathon.

Kwa Nini Saifee Marathon?

Saifee Marathon ni juhudi yetu ya kuwaleta pamoja Watanzania kutoka kila kona ya nchi yetu kwa lengo la kuleta mabadiliko katika vita dhidi ya saratani ya matiti. Fedha tunazokusanya kutoka marathon hii zitalenga kusaidia wagonjwa 100 kupata matibabu sahihi ya upasuaji wa saratani ya matiti. Tunaamini kwamba kwa umoja wetu na mshikamano, tunaweza kuokoa maisha na kuleta mabadiliko katika jamii yetu.

Tukutane Greenpark ( Uwanja wa farasi) Oysterbay Tarehe 8 Octoba 2023

Tunawakaribisha nyote kujiunga nasi katika matembezi haya ya mwanga, ambayo yataanzia Greenpark tarehe 08 -10-2023. Hii ni fursa ya kuonesha mshikamano wetu na kujitolea katika kuelimisha jamii yetu kuhusu umuhimu wa kugundua saratani ya matiti mapema na kusaidia wagonjwa kupata matibabu wanayohitaji.

Tunajivunia kuwa sehemu ya harakati hii ya kuokoa maisha, na tunakualika kujiunga nasi kwa kusajili na kushiriki katika Saifee Marathon. Pamoja, tunaweza kuwasha taa la elimu na ushindi dhidi ya saratani ya matiti.